Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Watu saba wa familia moja wafa maji Ziwa Victoria

Watu saba wa familia moja wafa maji Ziwa Victoria

Misungwi. Watu saba wa familia moja wamekufa maji na wengine wanne kunusurika baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kupinduka na kuzama Ziwa Victoria wilayani hapa Mkoa wa Mwanza. Familia hiyo ya watu 11 ilikuwa ikisafiri kutoka Kijiji cha Lubili wilayani Misungwi kwenda kwenye kikao mkoani Geita. Mmoja wa walionusurika kwenye ajali hiyo, Juma Maguta (50), alisema ajali hiyo ilitokea Jumanne wiki hii baada ya mtumbwi huo kupigwa na dhoruba. “Hali ya hewa Ziwa Victoria ilikuwa shwari, tulipofika katikati upepo mkali ulizuka na mtumbwi kupigwa na mawimbi mawili na kuzama,” alisema Maguta. Alisema baada ya mtumbwi huo kuzama, watu wanne kati yao, walipiga mbizi na kufanikiwa kujiokoa, huku wengine wakizama na kufa. Maguta alisema yeye na wenzake watatu waliokolewa na boti ya wavuvi iliyokuwa ikitokea Geita. Aliwataja wengine walionusurika kuwa ni Silvanus Charles (39), Ngabo Ngalu (39) na Vena Ramadhani (40), wakazi wa Lubili. Waliokufa ni pamoja na mtoto wa miaka mitat...