Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mbaroni Kwa Kukutwa Wakitoa Mamilioni Kwa ATM Za Watu 19

Mbaroni Kwa Kukutwa Wakitoa Mamilioni Kwa ATM Za Watu 19

Picha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa wanatoa fedha benki ya NMB tawi la Mpanda kiasi cha shilingi 3,680,000 wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi hizo. . Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi Damasi Nyanda amesema watuhumiwa hao watatu walikamatwa jana majira ya saa tatu usiku katika Tawi la NMB Mpanda . Watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa upelelezi bado unaendelea, wamekamatwa na askari wa jeshi la polisi waliokuwa wakilinda Benki hiyo. Nyanda ameeleza kuwa watumiwa walikamatwa baada ya askari polisi kuwatilia mashaka kutokana na kuwaona wakiwa wamekaa muda mrefu kwenye chumba cha mashine ya kutolea fedha . Amesema baada ya kuwatilia mashaka polisi waliingia ndani ya chumba hicho na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wanaendelea kutoa fedha katika mashine tatu zilizomo kwenye mashine za kutolea fedha. Kaimu Kamanda alieleza ndipo askari polisi walipoamua kuwapekua watu...