Mwanaume Shoga Aamua Kukiri Redioni Kufanya Biashara Hiyo...Aangua Kilio na Kuelezea A to Z Jinsi Alivyoanza....Ataka Kuacha
Morogoro: My confession! Katika hali isiyo ya kawaida, kijana Karimu Said (25) almaarufu Anti Karimu aliyekiri kufanya biashara haramu ya kuuza mwili (ushoga), ameangua kilio redioni wakati akiutangazia umma wa Watanzania kuachana na dhambi hiyo aliyodumu nayo kwa miaka saba. Ilikuwa Alhamisi iliyopita, Karimu alifika katika ofisi ndogo za gazeti hili za mkoani hapa na baadaye alitinga kwenye Kipindi cha Mcharuko wa Pwani cha Radio Planet FM kinachoendeshwa na mtangazaji mahiri, Warda Makongwa akishirikiana na Farham Abraham. Lengo la Karimu lilikuwa ni kutubu dhambi yake hiyo sambamba na kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu na Watanzania kwa jumla. Akiwa hewani laivu kwenye kipindi hicho na watangazaji hao na mwandishi wetu, Karimu alisimulia kilichomwingiza kwenye ushoga kuwa ni umaskini uliotokana na vifo vya wazazi wake. “Baada ya wazazi wangu kufariki dunia na mimi kumaliza darasa la saba hapa Morogoro, nilikwenda Dar kutafuta kazi. Nilipofika nilipat...