SIMBA YAMUWASHIA KESSY TAA YA KIJANI KWENDA ANAKOTAKA
Ramadhani Kessy-Beki wa Simba SC Uongozi wa Simba umemuwashia taa ya kijani beki wake wa kulia Hassan Kessy baada ya nyota huyo kusema hatoendelea kutoa huduma yake kwenye klabu hiyo baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa golikipa wake Mu-Ivory Coast Vicent Agban baada ya Kessy kutolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu wakati wa mchezo wa VPL kati ya Simba dhidi ya Toto Africans. Afisa habari wa klabu hiyo amekaririwa na kituo kimoja cha radio akisema Kessy ameikuta Simba na ataondoka na kuiacha hivyo kama ameamua kuondoka asubiri hadi mkataba wake utakapomalizika aachane na klabu hiyo. “Sisi tunafahamu Kessy bado tunamkataba naye kama ataamua kuiacha Simba, Simba siyo ya babayake wala ya mamayake anaweza akaenda popote anapotaka tunamruhusu lakini atomize majukumu yake amalize mkataba wake, lakini kama kaamua hivyo sawa maisha yataendelea tu hata akiondoka Simba bado itaendelea kuwepo”, anasema Manara afisa habari wa klabu ya Simba SC. Agban alimchapa makonde Kessy akimtu...