Mkuu wa Mkoa wa Lindi Amtumbua JIPU Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
Serikali ya Mkoa wa Lindi imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Oliver Vavunge na kumwomba Waziri Mkuu amsimamishe kazi Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Kilimo cha Umwagiliaji Maji Taifa kutokana na hasara ya Sh milioni 500 katika mradi wa umwagiliaji maji wa Kiwalala Narunyu, Lindi. Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliyasema hayo jana wakati alipozungumza na wananchi kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Kiwalala wilayani humo juzi. Zambi alisema kati ya fedha zilizowekwa kwa ajili ya kutekeleza mradi wa umwagiliaji maji ni Sh milioni 700, kati ya hizo Sh milioni 500 zilishatumika na kubakia Sh milioni 200. Alisema mradi huo ulioanza mwaka 2011 mpaka mwaka huu haujakamilika na fedha zilishachukuliwa, na kufafanua kuwa mkurugenzi anaingia hatiani kutokana kutokuwa makini juu ya mradi huo katika usimamizi. Alitoa fedha kwa nyakati tofauti kumlipa mkandarasi wa kwanza na kuvunja mkataba naye Sh milioni 121, wa pili alivunja na alitoa Sh milioni 226 ...