Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mpenzi wa zamani anavyoweza kukutibulia penzi lako la sasa

Mpenzi wa zamani anavyoweza kukutibulia penzi lako la sasa

Picha
T MEDIA NEWS Mahusiano KATIKA safari ya mapenzi kuna uwezekano mkubwa mtu akawa ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watu wengi kabla ya kumpata yule sahihi wa kuishi naye kama mke na mume. Rekodi zinaweza kutofautiana kutoka kwa mtu na mtu ila kama wewe umewahi kuwa na uhusiano na zaidi ya mtu mmoja huko nyuma, unatakiwa kuwa makini katika maisha yako ya sasa ili huyo mpenzi wako wa zamani asije akakutibulia. Tumekuwa tukishuhudia mikwaruzano ya hapa na pale kati ya wapenzi chanzo kikiwa ni mmoja kukuta aidha meseji isiyoeleweka kwenye simu ya mwenzake ikitoka kwa mpenzi wake wa zamani au unaweza kusikia mwanaume kamshushia kipigo mpenzi wake baada ya kumkuta akiwa katika mazingira tata na ‘mtu’ wake wa zamani. Hayo yamekuwa yakitokea kila siku lakini chanzo ni wengi kutojua jinsi wanavyoweza ‘kuwahendo’ wapenzi wao wa zamani na kuhisi hata wakiwa karibu nao hawawezi kuwa na madhara. Yawezekana ni kweli huyo mpenzi wako wa zamani hamkuachana kwa sha...