CBE YATOA UFAFANUZI TUHUMA ZA UPOSTOSHAJI.
Mkuu wa Chuo cha Elimu Biashara (CBE) Prof. Emmanuel Mjema akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ripoti ya Mamlaka ya Udhibiti ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ya Mwaka huu inayoonesha chuo hicho ni moja kati ya Taasisi 14 zilizofanya vizuri kwa kushika nafasi ya kwanza kwa kupata alama 95.8 katika kufuatilia sheria ya manunuzi ya umma na kuutaka umma kupuuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa wanakiuka sheria hizo. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO. Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emmanuel Mjema akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) inayoonesha kuwa chuo hicho kimepata ziada ya bilioni 1.2 kati ya mwaka huu na kufanya chuo kujiendesha kwa faida tofauti na baadhi taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari. ………………………………...