Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya aliyempa assists nyingi zaidi

Magoli 500 ya Messi: Uchambuzi wa kinamba, aliyempa assists nyingi zaidi, timu alizozifunga zaidi – bado hajamfikia CR7

Picha
  Lionel Messi jana usiku alitimiza magoli 500 tangu alipoanza kucheza soka la ushindani, wakati Barcelona ilipofungwa 2-1 nyumbani na Valencia.     Hii ni rekodi mpya kwa Messi na imekuja baada ya miaka 11, baada ya goli lake la kwanza akiwa na miaka 17 alilofunga dhidi ya Albacente mnamo May 2005.  Sasa tuangalie uchambuzi wa kinamba wa namna Muargentina huyu alivyofikisha idadi hii ya magoli kwa klabu na nchi yake.    Messi huanza mechi taratibu   Messi ni aina ya wqchezaji ambao huanza mechi taratibu, takwimu zinaonyesha ni magoli 50 tu kati ya 500 ambayo alifunga katika dakika 15 za kwanza za mechi – lakini amekuwa mwiba kwa timu pinzani kwa dakika nyingine 75 zinazofuatia. Huadhibu sana timu pinzani pale zinapoanza kuchoka.  Ni mguu mmoja tu wa Messi ambao ni hatari   Unataka kumzuia Messi asifunge? Mzuie asipige na mguu wake wa kushoto, unaweza kufanikiwa kwa asilimia 81%, kwa sababu asilimia 81 ya magoli yote aliyofunga a...