SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 18 Aprili 2016

T media news

Magoli 500 ya Messi: Uchambuzi wa kinamba, aliyempa assists nyingi zaidi, timu alizozifunga zaidi – bado hajamfikia CR7

 

Lionel Messi jana usiku alitimiza magoli 500 tangu alipoanza kucheza soka la ushindani, wakati Barcelona ilipofungwa 2-1 nyumbani na Valencia. 
  Hii ni rekodi mpya kwa Messi na imekuja baada ya miaka 11, baada ya goli lake la kwanza akiwa na miaka 17 alilofunga dhidi ya Albacente mnamo May 2005. 

Sasa tuangalie uchambuzi wa kinamba wa namna Muargentina huyu alivyofikisha idadi hii ya magoli kwa klabu na nchi yake. 

 Messi huanza mechi taratibu 
Messi ni aina ya wqchezaji ambao huanza mechi taratibu, takwimu zinaonyesha ni magoli 50 tu kati ya 500 ambayo alifunga katika dakika 15 za kwanza za mechi – lakini amekuwa mwiba kwa timu pinzani kwa dakika nyingine 75 zinazofuatia. Huadhibu sana timu pinzani pale zinapoanza kuchoka.

 Ni mguu mmoja tu wa Messi ambao ni hatari 
Unataka kumzuia Messi asifunge? Mzuie asipige na mguu wake wa kushoto, unaweza kufanikiwa kwa asilimia 81%, kwa sababu asilimia 81 ya magoli yote aliyofunga amefunga na mguu wa kushoto – magoli 406, wakati mguu wa kulia magoli 71, na kichwa magoli 21. Mipira ya adhabu ndogo – magoli 25 na penati 64. 

 Kwenye misimu 8 iliyopita amefunga wastani wa magoli 40 kwa msimu. 
Messi msimu huu mpaka sasa amefikisha magoli 42.  

Timu alizozifunga  
Atletico Madrid na Sevilla wana sababu za kumuogopa Messi zaidi – amezifunga magoli 25 kila timu. Magoli manne zaidi ya aliyoyafunga dhidi ya Real Madrid. 

 Mashindano aliyofunga magoli 
Magoli mengi zaidi amefunga katika La Liga. Wakati kwenye World Cup amefunga matano tu. 

 Amezidiwa na Cristiano Ronaldo 
Messi pamoja na mpinzani wake Ronaldo wamefunga jumla ya magoli 1,039. 

 Anahitaji kumpa zawadi Dani Alves 
Barcelona right-back Dani Alves ndio anaongoza kumpa Messi pasi za mwisho kabla ya kufunga, wamecheza pamoja kwa miaka 10. 

  
Messi alifanikiwa kuwa mchezaji pekee aliyefunga magoli matano katika mchezo mmoja wa Champions League wakati Barca ilipoifunga Bayer Leverkusen 7-1 mwaka 2012.