SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 29 Aprili 2016

T media news

MSANII RIYAMA ALLY ASEMA NILIKUWA NAPENDA UGOMVI NA "BEEF" SANA

Malkia wa filamu nchini, Riyama Ally amesema wakati akiwa mdogo alikuwa anapenda sana ugomvi.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti Alhamisi hii, Riyama alisema wakati huo watu mtaani kwao walikuwa wanamuogopa.

“Utotoni nilipenda sana ugomvi, yaani mtu asinichokoze ninaye huyo yaani nilikuwa napenda kupigana na kuingilia ugomvi hata kama haunihusu kiasi mtaani walikuwa wananiogopa, kitu ambacho nikikumbuka huwa najicheka mwenyewe,” anasema

Katika hatua nyingine muigizaji huyo amesema hakuwahi kufikiria kama angekuja kuwa muigizaji, kwani alikuwa anapenda sana kuimba taarab.

“Sio siri sikuwahi kuota kama ningekuwa kuwa mwigizaji, nilitamani sana kuwa muimbaji wa taarabu, muziki ninaoupenda mpaka leo,” anasema Riyama.

CHANZO na Bongo5.