Na Baraka Mbolembole
Mechi sita za ligi kuu ya kandanda Tanzania bara zitachezwa leo Jumamosi na siku ya kesho Jumapili katika miji tofauti. Kama ilivyo kawaida ya mtandao wako huu wa tawfiqmassin.blogspot.com leo tena tunakuja tofauti.
Kumbuka ni timu sita tu kati ya 16 za msimu huu zimewahi kushinda ubingwa VPL. Yanga, Simba, Mtibwa, Coastal, African Sports na Azam FC. Nimekuchambulia ligi yote na kukuwekea katika mtindo wa namba kuanzi namba moja (1) hadi 62.
Ni timu moja tu kati ya 16 zinazocheza Ligi kuu ndiyo itapata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Afrika hapo mwakani. Kwa mara ya kwanza katika historia bingwa pekee wa ligi ndiye atapaa kimataifa.Namba hii inamuwakilisha mlinzi namba mbili wa Azam FC, Shomari Kapombe ambaye amefunga magoli 8 katika VPL hadi sasa na kuwa kinara wa ufungaji upande wa wachezaji wa nafasi za ulinzi. Mlinzi huyo wa Taifa Stars amekosa michezo miwili iliyopita ya timu yake na atakosa pia michezo mitano ya mwisho kutokana na kuendelea kupata matibabu ya tumbo ambayo amegundulika kuwa nayo mwezi uliopita.Timu tatu za mwisho katika msimamo zitashuka daraja kutoka ligi kuu hadi ligi daraja la kwanza.Simba SC ndiyo timu pekee iliyopoteza michezo minne hadi sasa katika ligi kuu na huu ni msimu wao wa nne (4) wanapigania taji hilo tangu walipotwaa kwa mara ya mwisho msimu wa 2011/12.Nafasi waliyopo mabingwa wa zamani wa Tanzania timu ya Tanzania Prisons ya Mbeya. Hii ni nafasi ya juu zaidi kwa mabingwa hao wa ligi kuu ya Muungano mwaka 1999 ambao walitereka daraja msimu wa 2009/10 na kurejea tena msimu wa 2012/13. Prisons imekusanya alama 41 ambazo ni nyingi zaidi kwao tangu msimu wa 2007/08 walipomaliza katika nafasi ya pili.Kama msimu utamalizika katika mpangalio wa sasa (kabla ya game za wikendi hii,) Yanga SC, Azam FC, Simba, Mtibwa Sugar, Prisons na Mwadui FC moja kwa moja zitaunda bodi ya ligi kuu. Timu 6 za mwanzo katika VPL huingiza wajumbe katika bodi ya ligi. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu za Prisons na Mwadui FC kama zitasalia katika nafasi walizopo sasa (nafasi ya 5 na ile ya 6 upande wa Mwadui.)Nafasi waliyopo Stand United ya Shinyanga. Hiyo ni nafasi ya juu zaidi kwa timu hiyo katika historia yake VPL. Stand inacheza msimu wake wa pili katika VPL na ilinusurika kushuka katika siku ya mwisho ya msimu uliopita. Hadi sasa wana pointi 34 baada ya kucheza game 25.Msimu wa pili wa Ndanda SC si mbaya sana kama ule uliopita ambao walilazimika kupambana ‘kufa na kupona’ na kuishinda Yanga siku ya mwisho ya msimu wa 2014/15 ili kubaki VPL. Ikiwa nafasi ya nane na alama zao 33 timu hiyo ya Mtwara imepoteza game 8-timu pekee iliyopoteza mechi 8 hadi sasa na wana uhakika wa kutoshuka daraja hata kama watapoteza game zao tatu za mwisho. Hii ni nafasi ya juu zaidi kwao katika VPL.Majimaji FC ya Songea, Ruvuma iliteremka daraja kwa mara ya mwisho msimu wa 2010/11 baada ya kupoteza mechi ya mwisho dhidi ya Simba kwa kulazwa 4-1. Ikiwa imerejea tena VPL msimu huu timu hiyo haitashuka daraja hata kama itapoteza michezo yake minne iliyosalia. Ikiwa na alama 33, Majimaji imejikita katika nafasi ya 9 ya msimamo.Licha ya kutua kwa majina makubwa katika kikosi cha Mbeya City FC mambo yamekuwa magumu zaidi katika msimu wao wa 3 VPL. Timu hiyo ya Mbeya ilicheza ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu wa 2013/14 na kumaliza katika nafasi ya 3 ya msimamo.
Ikamaliza nafasi ya nne msimu uliopita. Na baada ya kuwapoteza nyota wake wengi kama Deus Kaseke, Peter Mwalyanzi, Anthony Matogolo kisha baadae kocha waliyedumu naye kwa miaka minne, Juma Mwambusi, timu hiyo ya Manispaa ya jiji la Mbeya licha ya kuwasaini wachezaji wazoefu kama kipa Juma Kaseja, Ramadhani Chombo, Haruna Moshi, Joseph Mahundi, Tumba Sued, Haruna Shamte.
Kisha makocha Meja Mingange aliyechukua nafasi ya Mwambusi kabla ya kutimuliwa na kuwa chini ya Mmalawi, Kinnah Phiri bado wameshuka hadi nafasi ya kumi-nafasi yao mbaya zaidi katika historia ya VPL tangu walipopanda mwaka 2013.
Namba ya jezi ya mshambulizi wa Yanga raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma. Akiwa tayari amefunga magoli 14 hadi sasa katika VPL, Ngoma anahitaji kufunga magoli matatu tu ili kufikia rekodi ya magoli 17 katika msimu wake wa kwanza VPL akiwa mchezaji wa kigeni.
Mkenya, Boniface Ambani alifunga jumla ya magoli 17 katika msimu wake wa kwanza katika ligi kuu Bara akiwa na kikosi cha Yanga msimu wa 2008/09. Mrundi, Amis Tambwe akafunga magoli 19 alipotwaa tuzo ya ufungaji bora akiwa mchezaji wa Simba msimu wa 2013/14. Ngoma ataweza?
Nafasi waliyopo Kagera Sugar ya Bukoba. Kuanzi nafasi waliyopo hadi ile ya mwisho ye yote atashuka daraja na kama timu hii itashuka itakuwa ni kwa mara ya kwanza tangu walipocheza msimu wao wa kwanza mwaka 2006 baada ya kuwa chini ya umiliki wa kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar. Wana pointi 25 baada ya kucheza michezo 27.Nafasi waliyopo JKT Ruvu ya Pwani timu ambayo haijawahi kushuka daraja tangu walipopanda kwa mara ya kwanza mwaka 2002. Ikiwa imecheza game 25, Ruvu wanaweza kushuka kama hawatafanya jitihada kwani wapo juu ya timu ya mwisho katika msimamo kwa tofauti ya alama mbili tu.Nafasi ya mwisho kwa timu tatu ambazo zitashuka daraja kwenda FDL msimu ujao. Hadi sasa nafasi ya 14 katika msimamo inashikikiliwa na timu ya JKT Mgambo ya Tanga ambayo imekusanya pointi 23 katika michezo yao 26 waliyokwisha cheza hadi sasa.Baada ya miaka 23 katika ligi za madaraja ya chini mabingwa wa Tanzania wa mwaka 1988, timu ya African Sports ya Tanga ilirejea ligi kuu Bara msimu huu lakini michezo mitatu waliyobaki nayo katika ligi huenda isiwabakize katika ligi hata kama watapata ushindi. Ikiwa nafasi ya 15 ya msimamo, Sports imekusanya alama 23 sawa na Mgambo. Je, watapanda na kushuka?Nafasi ya mwisho kabisa katika ligi inashikiliwa na mabingwa wa mwaka 1988 wa ligi hiyo, timu ya Coastal Union ambayo imekusanya pointi 22 katika game 27.Nahodha wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditti anacheza msimu wake wa 17 mfululizo katika ligi kuu Bara. Kwa mara ya kwanza, Nditti alicheza ligi kuu bara mwaka 1999 akiwa na kikosi cha Singida United ya mkoani Singida.
Alijiunga na Mtibwa mwishoni mwa mwaka 2000 ambako alicheza hadi mwaka 2004 alipojiunga na Simba. Akarudi tena Mtibwa mwaka 2005 na kudumu hapo hadi sasa. Ni mchezaji mzuri bado na ana nguvu ya kushinda na vijana wa sasa.
Amis Tambwe alifunga magoli 19 msimu wa 2013/14, akafunga tena magoli 15 msimu uliopita na hadi sasa amekwishatupia kambani magoli 18.Hamis Kizza alicheza VPL kwa mara ya kwanza msimu wa 2011/12 aliposajiliwa na Yanga akitokea kwao Uganda. Alidumu Yanga hadi katikati ya mwaka 2014 na baada ya kumalizika kwa mkataba wake akaenda kucheza barani Asia kisha Simba wamemrejesha VPL msimu huu.
Mganda huyo yuko karibu kushinda tuzo ya ufungaji bora kwa mara ya kwanza. Ndiye kinara wa ufungaji hadi sasa akiwa amekwisha funga magoli 19.
Azam FC imefunga jumla ya magoli 43 katika game 25 msimu huu. Magoli 20 yamefungwa na washambuliaji wake-pacha, Mu-ivory Coast, Kipre Tchetche na nahodha wa timu, John Bocco ambao kila mmoja amefunga magoli kumi.Licha ya kutopoteza mchezo katika uwanja wake wa nyumbani, Sokoine, Mbeya timu ya Prisons imeruhusu jumla ya magoli 21 katika michezo yao 26. Idadi ya juu zaidi miongoni mwa timu 5 za juu wakati JKT Mgambo ikiwa imefunga magoli 21-idadi ya juu zaidi ya timu 3 za chini katika msimamo.Stand United imefunga magoli 22 na kuruhusu 22 hivyo wana wastani wa magoli 0.Idadi ya magoli yaliyofungwa na Prisons hadi sasa katika VPL.Idadi ya magoli ya kufunga yaliyofungwa na timu ya JKT Ruvu katika ligi.Timu mbilitu zimefunga jumla ya magoli 25 hadi sasa. Mwadui FC na Toto Africans.Idadi ya magoli yaliyofungwa na Ndanda SC katika game zao 27.Wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa ya Azam FC. Wamefunga 43 na kuruhusu nyavu zao mara 16 katika game 25.Idadi ya magoli ya kufunga ya Mbeya City FC.Ni wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa ya Simba. Ikiwa imefanikiwa kufunga jumla ya magoli 43 hadi sasa Simba wameruhusu nyavu zao mara 14 na kufanya wawe na wastani wa magoli 29.Kila timu itacheza michezo 30 msimu huu, mechi 15 za mzunguko wa kwanza na nyingine 15 za mzunguko wa pili.Kagera Sugar imeruhusu magoli 31 katika ligi hadi sasa.Timu za Ndanda SC na Majimaji FC zimekusanya pointi 33 kila timu baada ya kucheza game 27.JKT Mgambo imeruhusu jumla ya magoli 34 hadi sasa.Hakuna timu yenye pointi 35 hadi sasa katika VPL.Timu tatu zimeruhusu magoli 36 hadi sasa nazo ni Majimaji, Toto Africans na Coastal Union.
38 JKT Ruvu ndiyo timu iliyoruhusu magoli mengi zaidi katika VPL hadi sasa, wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara 38.
Wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa ya timu ya Yanga ni 45. Wamefunga magoli 59 na kuruhusu 14 tu katika nyavu zao.Huu ni msimu wa 53 wa ligi kuu Tanzania Bara.Simba imekusanya pointi 57 hadi sasa ni idadi ya juu zaidi kwao tangu waliposhinda ubingwa wao wa mwisho Mei, 2012.Azam FC wamekusanya alama 58 katika game zao 25.Yanga ndiyo timu iliyofunga magoli mengi zaidi hadi sasa, wamefunga jumla ya magoli 59 katika mechi 25 walizokwisha cheza.Yanga ndiyo wanaongoza msimamo wa ligi wakiwa wamekusanya alama 62 na wana game 5 kabla ya kumaliza kwa msimu.