SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 29 Aprili 2016

T media news

STAA WOLPER AOGOPA KUWEKA WAZI MAHUSIANO YA KIMAPENZI.

Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amesema kwamba siyo vizuri kuzungumzia masuala ya mchumba wake kwenye vyombo vya habari au kujitangaza sana kwani mtu unaweza kuishia kwenye kuvishwa pete ya uchumba tuu.

Akizungumza katika kipindi cha Nirvana cha East Africa Television Jumanne hii, Wopler alisema mpenzi wake wa sasa ambae alivalisha pete siyo mume wa mtu kama watu wanavyodai.

“Mimi sipendi kuzungumzia masuala ya mahusiano yangu na mchumba wangu kwenye vyombo vya habari,” alisema Wolper.”Kwani huweza kutokea mtu akaishia kwenye ‘engagement ring’ hivyo nitasema nikashaolewa na siyo sasa,”

Pia Wiopler alisema kwamba mchumba aliye naye kwa sasa alianza kumtongoza toka mwaka 2012 akakataa ila mambo yalivyoenda ndivyo sivyo kwa mchumba wa awali ikabidi amsikilize huyu ambaye yupo naye kwa sasa.

CHANZO na Bongo5