SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 29 Aprili 2016

T media news

TWAWEZA: 80% YA WATANZANIA WANAAMINI RAIDO..???


Asilimia 91 ya wananchi waliohojiwa wanaitaka Serikali kabla ya kukifungia chombo chochote cha habari ni vema kukifikisha chombo hicho mahakamani ili kutoa fursa ya suala hilo kupitia hatua za kisheria kuliko ilivyo sasa.

Mapendekezo hayo yametolewa katika ripoti ya utafiti wa wananchi juu ya haki ya kupata habari iliyofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali ya TWAWEZA ikionyesha kuwa wananchi wengi wanaunga mkono suala la uwazi na uwajibikaji na kuwa upatikanaji wa habari huzuia vitendo vya rushwa.

Akiongea wakati wa uwasilishwaji wa ripoti hiyo kwa waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, mshauri mwandamizi wa mawasiliano wa tasisi ya TWAWEZA Risha Chande amesema, 

Takribani wananchi kati ya wanane na kumi ambao ni sawa na asilimia 78 wanaamini upatikanaji wa habari unapunguza vitendo vya rushwa, huku wanachi kati ya sita na kumi ambao ni sawa na asilimia 68 wamependekeza serikali iwe na mamlaka muhimu ya kuzuia habari zinazotishia usalama wa Taifa.

Aidha, ripoti hiyo pia iligusia hali ya upatikanaji wa habari kutoka taasisi za umma kwa wananchi ambapo zaidi ya wananchi kati ya wanane na kumi walio hojiwa katika ripoti hiyo wamesema hawajawahi kufika katika ofisi za mamlaka ya Maji, shule za Umma, vituo vya Afya wala ofisi za serikali za mitaa kutafuta taarifa zozote nakuwa wananchi wengi wakitegemea vyombo vya habari mbalimbali kupata taarifa kutoka taasisi hizo.

Richa amesmea Redio inaaminika na asilimia 80 ya wananchi, runinga (TV) inaaminika na asilimia 73 ya wananchi, tofauti na magazeti ambayo yanaaminika kwa asilimia 27 tu ya wananchi. Japokuwa mitandao ya kijamii inaaminika kwa kiasi kidogo sana na kutumiwa kwa kiwango cha chini kama chanzo cha habari.