SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 29 Aprili 2016

T media news

Tiba ya miezi 4 kwa wagonjwa wa kifua kikuu yaja

Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIMR kituo cha Mbeya imesema ipo katika hatua ya tatu ya kugundua tiba ya Kifua Kikuu itakayo tumiwa na waathirika wa ugonjwa huo kwa miezi 4 kutoka miezi 6 ya sasa.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu tafiti mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo juu ya magonjwa mbalimbali Mkurugenzi wa Tehama na Mtafiti Mkuu Kiongozi Dk. Leonard Mboera amesema tafiti hiyo ilianza mwaka 2015 na hatua iliyofikiwa ni kuchunguza ubora na usalama wa mchanganyiko wa dawa zilizotumika katika tiba hiyo.

Aidha Dk. Mboera amesema ili kubaini maambukizi ya Kifua Kikuu katika muda mfupi ni vyema kifaa cha GenXpert MTB/RIF kikatumiwa kama ilivyoainishwa na Shirika la Afya Duniani katika Hospitali za Mikoa na Wilaya kwani tafiti zinaonyesha uwezo mkubwa wa kifaa hicho kubaini virufi vya Kifua Kikuu.

NIMR Mkoa wa Mbeya pia imefanikiwa kutumia maabara inayotembea ili kuharakisha huduma ya upimaji wa virusi vya Ukimwi (VVU) na Kifua Kikuu sambamba na kutoa elimu kwa makundi hatarishi kupata maambukizi ya VVU.