SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 29 Aprili 2016

T media news

Beyonce aanza ziara ya Formation Miami, amshukuru mumewe

Mwishoni wa show hiyo, Queen Bey alimshukuru mume wake, Jay Z kwa kumuita ‘beautiful husband.’

Ndoa ya muimbaji huyo imekuwa kwenye mjadala tangu aachie album yake Lemonade yenye ujumbe wa kusalitiwa. Wimbo Sorry una mashairi ya kusalitiwa na mume wake na mstari usemao, ‘Becky with the good hair’ umesababisha mjadala mkubwa.

Wakati huo huo Jay Z alionekana akiwa ametulia kabisa mchana wa Jumanne huko Miami na pia alikuwepo kwenye rehearsal ya mke wake kwenye ukumbi wa Marlins Park.

Wawili hao wanaonekana kuwa katika hali nzuri licha ya mashairi makali kwenye Lemonade kama ‘This is your final warning … . If you try this s— again, you gon’ lose your wife.’