SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 29 Aprili 2016

T media news

Treni ya Deluxe kwenda Bara kuanza keshokutwa


Treni  ya abiria ya Deluxe kutoka Dar es Salaam kwenda Bara itaanza safari keshokutwa kwenda Kigoma baada ya kusimama kwa muda.

 

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli (TRL), Masanja Kadogosa, treni itaondoka asubuhi.

 

Kuanza kwa safari kunatokana na kutengamaa kwa eneo korofi baina ya stesheni za Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma.

 

Wakati pia safari za treni ya kawaida zitaanza kulingana na ratiba yake, kwa upande wa treni ya Deluxe inaondoka Dar es Salaam kila Jumapili saa 2.00 asubuhi.

 

Safari ya treni ya kawaida imepangwa kuanza Mei 3, mwaka huu. Mara ya mwisho huduma za treni za abiria ya kawaida zilihamishiwa Dodoma Aprili 07, mwaka huu.