Rais Shein Awaapisha Makatibu Wakuu Na Naibu Katibu Wakuu Wa (SMZ)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein jana aliendelea na hatua ya kuwaapisha makatibu wakuu wa wizara aliowateua juzi. Walioapishwa katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Vuga mjini Zanzibar ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee na naibu wake, Salmin Amour Abdulla. Wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Radhia Rashid Haroub na Naibu katibu wake, Bushiri Mbarouk, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Asha Ali Abdulla na manaibu wake, Yakout Hassan Yakout na Kubingwa Mashaka Simba. Wengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Joseph Abdalla Meza na naibu wake, Ahmed Kassim Haji. Khamis Mussa Omar aliapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na naibu wake Ali Khamis Juma. Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko ni Bakari Ha...