Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Serikali Yawatoa Wasiwasi Wananchi Kuhusu Uhaba wa Mafuta ya Ndege

Serikali Yawatoa Wasiwasi Wananchi Kuhusu Uhaba wa Mafuta ya Ndege

Picha
SERIKALI imewatoa wasiwasi Watanzania kuhusu taarifa za kutokea kwa uhaba wa mafuta ya ndege, uliokuwa ukitishia kusimama kwa usafiri huo muhimu kwa nchi. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema hayo bungeni jana jioni wakati alipokuwa akihitimisha mjadala wa Bajeti ya wizara hiyo, alipokuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo). Awali Zitto katika hoja yake, alisema kuwa akiba ya mafuta ya ndege nchini imebaki ya siku tano, jambo linaloweza kusababisha ndege za kimataifa kushindwa kutua nchini. “Zimebaki siku tano mafuta ya ndege aina ya JET AI kumalizika nchini baada ya mafuta yote kugundulika kuwa yamechafuka. Sasa baada ya siku hizo, ndege hazitatua nchini na itakuwa ni aibu na nchi itakosa fedha za kigeni kwa watalii kutokuja nchini,”  alisema Zitto. Alisema anazo barua kutoka kwa Wakala wa Kuagiza Mafuta kwa Pamoja na alikuwa tayari kuziwakilisha kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhong...