Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Bungeni: Serikali yaanza Kuzipanga Shule Katika Makundi ili Kuweka Viwango vya Ada Elekezi

Bungeni: Serikali yaanza Kuzipanga Shule Katika Makundi ili Kuweka Viwango vya Ada Elekezi

Picha
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, imeanza zoezi la kupanga shule katika makundi ili kuweka viwango vya ada kwa kuzingatia ubora wa huduma na kwamba haitaathiri ubora wa elimu. Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, aliyasema hayo wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema).  Mdee alitaka kufahamu iwapo Serikali imebaini kiwango cha gharama kwa kila mwanafunzi kwa shule za bweni na kutwa, iwapo hakitasababisha kuporomoka kwa ubora wa elimu. Manyanya alisema wizara hiyo imefanya utafiti kuhusu gharama za kila mwanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari.  “Baada ya utafiti, wizara yangu ilifanya mazungumzo na baadhi ya taasisi zinazosimamia elimu kwa shule zisizokuwa za Serikali na kukubaliana jinsi ya kufikia viwango vya ada elekezi,” alisema. Alisema wizara inatarajia ubora wa ada elekezi hautaathiri elimu kwa shule binafsi, kwa sababu itapangwa kulingana na ubora wa miundombinu ya shule. Katika swali la nyonge...