CHADEMA – RAIS MAGUFULI NI MKWAPUAJI
DODOMA CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema, Rais Dk. John Magufuli ni mkwapuaji. Kimeeleza, Rais Magufuli amekwapua sera za chama hicho kwa pupa lakini hana uwezo wa kuzitekeleza kwa kiwango kinachokubalika. Pia kimeeleza, Rais Magufuli anatokana na chama chenye misingi ya wizi na kwamba, serikali yake chini ya uongozi wa (CCM) haiwezi kuwa na safi. Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma na Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa Dk. Vicent Mashinji, wakati akifungua kongamano la Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) na Umoja wa Wanachadema Vyuo Vikuu (CHASO). Katika hotuba yake Dk. Mashinji amedai kuwa, Rais Magufuli amekuwa akifanya maigizo ya utumbuaji majipu kwa baadhi ya watumishi ili kuwaaminisha Watanzania kwamba kazi anayoifanya ni sahihi. Hata hivyo amesema, Chadema hawapingi utumbuaji wa majipu na kwamba ni lazima utumbuaji huo ufuate sheria na kanuni za utumishi wa umma. “Nawakumbusha masuala ya haki, hakuna haki bila wajibu. Watawala wanatuongelea sisi, mbona...