Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Hofu Yatandaa Shkuba Kinara wa Madawa ya Kulevya Kutoroka Gerezani

Hofu Yatandaa Shkuba Kinara wa Madawa ya Kulevya Kutoroka Gerezani

Picha
Kufuatia kuendelea kushikiliwa kwa kigogo anayedaiwa kujishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya ‘unga’, Ali Khatib Haji ‘Shkuba’ (pichani) katika Gereza Kuu la Mkoa wa Lindi, hofu imezidi kutanda kwa madai kwamba, mfanyabiashara huyo yupo kwenye maandalizi ya kutoroka gerezani hapo, Uwazi limechimba kwa kina.  BOMBA LA MAJI LATAJWA   Habari zilizolifikia gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita na kutiliwa nguvu na hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea gereza hilo, zilieleza kwamba, kuna ‘mchongo’ unaofanywa na vigogo kadhaa wa unga kwa lengo la kumtorosha Shkuba, wakitumia kivuli cha mradi wa kuingiza bomba la maji gerezani hapo ambapo pengine hata wenye mradi huo hawajui lolote.  “Kuna bomba linachimbwa kuingia gerezani, wenyewe wanasema ni mradi wa kulipatia gereza hilo maji lakini kuna tetesi kwamba huenda bomba hilo ndiyo njia ya kutaka kumtolea Shkuba gerezani lakini wenye mradi hawana habari.  ...