Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Waliopata divisheni 0 hawapo kwenu tu hata kwetu wapo

Waliopata divisheni 0 hawapo kwenu tu hata kwetu wapo

Picha
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. MATOKEO ya Kidato cha Nne yametangazwa, shule zilizoaibika kwa matokeo mabaya ni za serikali zinazosomesha watoto wa maskini. Tukioanisha mantiki, ufaulu wa wanafunzi miaka ya hivi karibuni ni sawa na vita ya matajiri na maskini; mwaka huu tena walalahoi wamevuna aibu ya ufukara wao. NANI MWENYE KUJALI KATIKA HILI? Wakati mwingine fikra ni kitu cha ajabu, ndiyo maana katika muktadha huu wa matokeo mabaya ya shule nyingi za wasio nacho ni wachache waliotafakari taifa letu linaelekea wapi? Ni wazi kabisa, taifa lipo kwenye mtikisiko mkubwa wa ki-hali! Maisha na mafanikio bora yanachukuliwa mikononi mwa maskini walio wengi  na kurasimishwa kwa matajiri wachache.  Fedha hivi sasa inaongea! Ukitaka elimu bora, tiba nzuri, huduma za kijamii za kisasa usitumie kinywa chako; mfuko uteme noti; kila kitu ni murua! Hata nafasi za kisiasa bila fedha hupati. Nawasihi Watanzania wenzangu, tusikubali ...