CCM Iringa Vijijini watumbua majipu
Iringa. Chama cha Mapinduzi ( CCM ) Iringa vijijini mkoani hapa kimewavua uongozi na kuwasimisha uanachama, wanachama 23 kwa madai ya kuwa walikisaliti chama hicho wakati wa kampeni na uchaguzi mkuu wa Rais, ubunge na madiwani wa mwaka 2015. Wakati chama kikiwavua uongozi na uanachama makada hao, Baraza la Umoja wa Wanawake UWT wilayani ya Iringa Vijijini pia limewafukuza viongozi watano wa ngazi ambao ni makatibu wanne na mwenyekiti mmoja kwa tuhuma za usaliti. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Vijijini, Dodo Sambu alisema kupitia chama kimezingatia kaninu na taratibu za chama katika kufikia uamuzi wake wa kuwavua uongozi na uanachama viongozi hao. Alisema kanuni ya maadili ya uongozi ya 2010/12 ndiyo iliyotumika katika kuwachukulia hatua wanachama hao kwani kanuni hiyo inasema kuwa usaliti kwenye chama ni kosa hivyo kupitia kanuni hiyo na kuitisha halmashauri kuu wa wilaya ndiyo iliyoamua kuwavua uongozi na uanachama b...