SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 4 Machi 2016

T media news

CCM Iringa Vijijini watumbua majipu

Iringa. Chama cha Mapinduzi ( CCM ) Iringa vijijini mkoani hapa kimewavua uongozi na kuwasimisha uanachama, wanachama 23 kwa madai ya kuwa walikisaliti chama hicho wakati wa kampeni na uchaguzi mkuu wa Rais, ubunge na madiwani wa mwaka 2015.

Wakati chama kikiwavua uongozi na uanachama makada hao, Baraza la Umoja wa Wanawake UWT wilayani ya Iringa Vijijini pia limewafukuza viongozi watano wa ngazi ambao ni makatibu wanne na mwenyekiti mmoja kwa tuhuma za usaliti.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Vijijini, Dodo Sambu alisema kupitia chama kimezingatia kaninu na taratibu za chama katika kufikia uamuzi wake wa kuwavua uongozi na uanachama viongozi hao.

Alisema kanuni ya maadili ya uongozi ya 2010/12 ndiyo iliyotumika katika kuwachukulia hatua wanachama hao kwani kanuni hiyo inasema kuwa usaliti kwenye chama ni kosa hivyo kupitia kanuni hiyo na kuitisha halmashauri kuu wa wilaya ndiyo iliyoamua kuwavua uongozi na uanachama baada ya kupata ushahidi wa kutosha.

“Kiongozi yeyote ama mwanachama anayeshirikiana na wapinzani kuchimba na kukivuruga chama chetu huyo hawezi kukubalika kuwa miongoni mwetuna adhabu yake ni kufukuzwa unachama ndani ya chama”.

“Kwa mujibu wa kanuni wao ni wasaliti na kama wasaliti hawaitaji kubaki ndani ya uongozi au chama kwani wengine walionekana wakiwa wamevaa sare za chama cha Chadema na walionekana kufanya kampeni bila ya vificho, wengine walikuwa mawakala wa vyama vya upinzani … ukiwa wakala maana yake umeasi chama kingine’alisema.

Sambu aliwataja wanachamawaliovuliwa uongozi na kufukuzwa uanachamakuwa ni makatibu kata watano ,makatibu wenezi wawili na wajumbe wa kamati ya siasa wa kata tatu ambao jumla yao ni 15 pamoja na Mwenyekiti wa tawi ,alisema watu hawa walikuwa wanakaa kwenye vikao vya ndani vya maamuzi vya wilaya lakini walipeleka taarifa upinzani.

Alisema watuhumiwa hao ni wale waliokuwa kwenye kata nne ambazo zimeshindwa katika uchaguzi mkuu kwa ngazi ya udiwani ambazo ni Mgama, Kiwele, Ifunda, Migoli na kata moja ya Itunundu ambayo chama chake kilishinda kwa tabu huku katibu huyo akituhumiwa kuchelewesha barua za mawakala hadi saa tano ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi.

Katika hatua nyingine UWT iliwatimua viongozi watano waliosimaishwa uongozi baada ya kuhudhuria kikoa cha baraza maalumu lawanawake wilayani humo.

Katibu wa UWT wilaya ya Iringa Vjijini, Asha Stambuli akiongea katika kikao hicho alisema lazima wakisafishe chama cha chao kama anavyofanya Rais John Magufuli.

Aliwataja viongozi hao kuwa ni Leah Ibrahim Mwenyekiti wa UWT kata ya Kalenga,Josophina Choga Katibu UWT kata wa Nzihi,Tabu Mgeni Katibu UWT kata ya Ifunda,Betha Sanga Katibu UWT kata ya Kiwele na Kuruthum Kikwembe Katibu UWT Ilolompya.

Akiuzngumza mara baad aya kutimuliwa kwenye kikao Ibrahimu ambaye alikuwa mwenyekiti wa UWT kata ya Kalenga alisema yeye hakuwahi kushiriki kukihujumu chama na kwamba wamemuonea kwakumfukuza.