Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ethiopia

Kongamano la usalama barani Afrika lafanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia

Picha
Kongamano la usalama barani Afrika lenye kaulimbiu ya 'Afrika katika Ajenda ya Usalama wa Dunia' na lenye lengo la kubadilishana mawazo na kuchunguza changamoto za usalama hususan vitisho vya ugaidi, lilianza hapo jana Jumamosi mjini Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia. Katika kongamano hilo la siku mbili ambalo limesimamiwa na Taasisi ya Utafiti kwa ajili ya Usalama na Amani iliyo chini ya Chuo Kikuu cha Addis Ababa na kuhudhuriwa na viongozi wengi wa nchi za Afrika, washiriki wamejadili kwa kina changamoto za usalama hivi sasa barani humo. Miongoni mwa mambo mengine yaliyojadiliwa katika kongamano hilo la ushirikiano, ni kuandaa mipango ya kudhamini usalama na amani barani Afrika sanjari na kupambana na umasikini. Ukweli ni kwamba suala la usalama hivi sasa limegeuka na kuwa tatizo kubwa kwa nchi za Kiafrika, ambapo ugaidi umekuwa jinamizi kwa nchi zote za dunia. Utajiri mkubwa wa nchi za Kiafrika, kuwepo viongozi dhaifu, hali mbaya ya kisiasa na nafasi maalumu ya kijografia,...