Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC ) Lakanusha Kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, linapenda kutoa taarifa sahihi juu ya taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na vyombo mbalimbali vya habari, pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu TPDC kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic. Ni vyema ikaeleweka kwamba, Akaunti ya ESCROW ni Akaunti maalumu inayoweza kufunguliwa baina ya Kampuni, Taasisi, au Mashirika mbalimbali ya binafsi na yale ya umma kwa matumizi maalumu. Lengo la Akaunti ya ESCROW ni kuhifadhi fedha au kupitisha malipo kwa ajili ya shughuli maalum ikiwemo miradi au kazi yoyote maalumu na malipo haya hufanyika baada ya pande mbili kuridhia. TPDC ilifungua Akaunti tatu za Esrow baada ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kutoa idhini kufunguliwa kwa akaunti kwenye Benki ya Stanbic, ikiwa ni moja ya masharti yaliyowekwa na mkopeshaji ili kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ya gesi asilia, kut...