Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Habari Motomoto

Ujumbe unaohisiwa kuwa wa Belle 9 unaomdis Diamond Platnumz

Picha
Usiku wa March 2 kuamkia March 3 jina la mkali kutoka Bongoflevani Belle 9 lilirudi kwenye headlines baada ya kuonekana kwa post katika mtandao wa Instagram inamdis Diamond Platnumz lakini baadae inadaiwa kufutwa na account ya msaani huyo kufanyiwa mabadiliko ya jina. Baada ya muda stori zilianza kuzagaa mitandaoni kuwa post hiyo sio ya kweli huku […] The post Ujumbe unaohisiwa kuwa wa Belle 9 unaomdis Diamond Platnumz

Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali Akamatwa..

Picha
Jeshi la Polisi  Mkoani Morogoro, wilayani Kilombero  jana  lilimkamata mbunge wa jimbo la Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali kwa madai ya kutaka kuingia katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kuapisha na kuchagua mwenyekiti na makamu wake wakati si mpigakura. Lijualikali alikamatwa nje ya ukumbi wa halmashauri na polisi na kuswekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Kilombero saa 3.48 asubuhi wakati akiingia kwenye ukumbi huo kama mmoja wa mashuhuda. Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilombero, Shabaan Mikongolo alisema mbunge huyo hakutendewa haki na polisi kwa kuwa alifika eneo hilo kushuhudia matukio ya kuapishwa kwa madiwani. “Ni kama kuna maelekezo yalitolewa kwa polisi kuwazuia wabunge, Lijualikali na Devotha Minja (Viti Maalumu – Chadema) na mwakilishi wa Katibu Mkuu Chadema kutoingia ukumbini lakini viongozi wengine wa Serikali ngazi ya mkoa na wilaya waliruhusiwa." Alisema Mikongolo Pia, polisi walizuia waandishi wa habari na kutaka ku...

Ajikata utumbo kwa kunyimwa chakula

Picha
Kakonko. Kijana mwenye umri wa miaka 30, amefanya tukio la kushangaza kwa kujipasua tumbo kwa wembe na kuukatakata vipande utumbo wake. Tukio hilo lilitokea Februari 28, katika Wilaya ya Kakonko, Kigoma. Mkazi huyo wa Kijiji cha Kinonko, Furaha John alifikia uamuzi huo baada ya jaribio la kujinyonga kwa kutumia kamba kushindikana. John ambaye anaelezwa kuwa ni mfanyabiashara wa pombe za kienyeji, aliamua kujiua kutokana na hasira za kudhulumiwa Sh35,000 na pia kunyimwa chakula na mkewe. Akisimulia mkasa huo, John ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo, alisema alirejea nyumbani akiwa na hasira za ‘kurushwa’ fedha zake na mfanyabiashara mwenzake. Alisema nyumbani nako alikutana na tukio la kunyimwa chakula na mkewe, jambo lililomuongezea hasira na kuona bora afe.  “Yaani nilitoka kazini nimekasirika baada ya mwenzangu kunidhulumu fedha zote za mauzo ya siku hiyo, nafika nyumbani mke wangu naye akaninyima chakula. Nikaona ni bora kufa kwa sababu sina haja ya...

Ndoto za ubingwa bye bye kama Arsenal wasipofanya hivi

Picha
Arsene Wenger mwenyewe amekubali kwamba wakali wake wamepata ukame wa kucheka na nyavu kwa muda kidogo. “Kuna vitu vingi sana navichambua na tunatakiwa kutafuta jibu la haraka. Hili swala lipo kichwani mwangu na ninakubali kwamba kuna ukame mkubwa wa ufungaji kwa washambuliaji wetu”, alisema Wenger. Fikiria kuanzia kwa Sanchez amecheza mechi 10 hajafunga hata mara moja, Giroud amecheza mechi 6 hajafunga hata mara moja, Walcott amecheza mechi 10 kafunga mara moja tu. Hawa ni baadhi ya wachezaji muhimu ambao wanategemewa kuwa wanatupia nyavuni mara nyingi kusaidia club. Ukame huu wa wafungaji una athari kubwa kwenye harakati za kutafuta ubingwa. Arsenal ipo kwenye nafasi nzuri ya kushinda ubingwa msimu huu ambapo hivi sasa wapo nafasi ya 3 wakiwa na points 51. Leo watacheza mechi ya ya 28 dhidi ya Swansea City. Kila timu inataka ushindi na huu utakua ni ushindi muhimu sana kwa Arsenal. Baada ya Welbeck kurudi vizuri ameogeza tumaini la Arsenal kuendelea kwenye harakati za kuuta...

RAIS MAGUFULI AONGOZA MKUTANO WA JUMIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Picha
Wakuu wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameikubalia Sudan Kusini kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo ya kikanda. Mkutano wa kilele wa Jumuiya hiyo jijini Arusha leo  Jumatano (Machi 2) umepitisha  pendekezo la baraza la mawaziri juu ya uwanachama wa Sudan Kusini na pia hali ya usalama nchini Burundi. Kikao hicho kilichodumu kwa muda wa takribani masaa matano kimelikubalia taifa hilo changa kabisa barani Afrika kuwa mwanachama wake wa sita, kuungana na Tanzania, Rwanda, Burundi , Uganda na Kenya. Rais  Magufuli  ambaye ndiye  mwenyekiti wa kikao hicho, amewaambia wajumbe wa mkutano huo wa kilele kwamba sasa "Sudan ya Kusini ni mwanachama halali wa jumuiya" hiyo. Mkutano huo pia umezungumzia kwa kina masuala ya maendeleo ndani ya jumuiya ikiwemo mipango ya kujengwa kwa viwanda vya nguo na bidhaa za ngozi ili kuondoa kabisa biashara ya uagizaji wa nguo kuukuu, maarufu kama mitumba, katika nchi hizo katika miaka michachache ijayo Mkutano ...