MOTO WA RAIS MAGUFULI WAWAKA KILA KONA,VIGOGO WAWARUDISHA WATOTO BONGO,
Rais Dk John Pombe Magufuli. Stori: Mwandishi wetu, Ijumaa Dar es Salaam: BAADHI ya vigogo ambao ni watumishi wa muda mrefu serikalini, wameamua kuwarudisha nyumbani watoto wao waliokuwa wakisoma nje, ili waendelee na masomo kutokana na staili ya kubana matumizi inayofanywa na serikali ya awamu ya tano. Kwa mujibu wa chanzo kilicho serikalini, mianya mingi iliyokuwa ikitumiwa na vigogo hao kupata fedha, kama vile semina, vikao, kongamano na safari kufutwa na hivyo kuwafanya waishi kwa vipato vyao halali. “Zamani kulikuwa na vyanzo vingi vya hela zaidi ya mshahara, mtu angeweza kupiga simu moja au mbili, tayari ameingiza fedha, lakini hivi sasa kila sehemu imebana, watu wanawarudisha vijana wao nyumbani kwa sababu siyo rahisi kumudu gharama za masomo kwa mishahara,” kilisema chanzo hicho. Chanzo hicho kilidai kuwa maofisa wa serikali hivi sasa wamekuwa waoga hata kuchukua pesa halali kwa hofu ya kutumbuliwa, kwani hakuna dalili kama spidi ya kubana matumizi inayochukul...