Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Sakata La Mauaji Ya Diwani Wa CUF Lachukua Sura Mpya

Sakata La Mauaji Ya Diwani Wa CUF Lachukua Sura Mpya

Mauaji ya kikatili ya Diwani wa Kata ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Sylvester Muliga (CUF), yameanza kuibua mambo mazito huku ikielezwa kuwa Ijumaa alikuwa awasilishe hoja kwenye Baraza la Madiwani kuhusu masuala ya ardhi. Muliga ambaye alifia Hospitali ya Kagondo alikopelekwa kwa matibabu baada ya kukatwa mapanga Jumapili usiku, imeelezwa kuwa katika kikao hicho ilikuwa aombe kuundwa kwa kamati ya kuchunguza uhalali wa maeneo makubwa ya ardhi yanayomilikiwa na watu wachache. Kwa mujibu wa mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Mazingira ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kasharunga, Khalid Swalehe, hoja hiyo ilikuwa iwasilishwe na Muliga na ilikuwa inaungwa mkono na madiwani wa kata zote zilizo na migogoro ya ardhi. Baada ya taarifa za kufariki dunia kwa diwani huyo, wananchi walivamia nyumba nane za watuhumiwa wanaodaiwa kutekeleza mauaji hayo na kuziteketeza kwa moto. Pia, walichoma moto mashine mbili za kusaga na kuharibu gari la mmoja wa wagombea wa udiwani katika Uchaguzi M...