RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA MAKTABA MPYA YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandala, Balozi wa China hapa nchini lu you Qing, maafisa wa kampuni ya Kutoka China ya Jiangsu Jiangdu wakiweka mchanga kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika Maktaba Mpya ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam UD mara baada ya kuwasili chuoni hapo. Maktaba hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandala, Balozi wa China hapa nchini lu you Qing, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na makamu wa Rais katika serikali ya awamu ya nne Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Spika Mstaafu Pius Msekwa mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi ...