MIX Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania limeguswa na hujuma kwa Rais Magufuli
Mei 8 2016 Jukwaa huru la Wazalendo Tanzania limekutana na Waandishi wa Habari Dodoma ili kutoa tamko lao kuhusu hujuma dhidi ya Rais John Pombe Magufuli. Katibu wa jukwaa hilo Mtela Mwampamba amesema ’Kwa miaka mingi Watanzania tumekuwa tukipiga kelele tukilia juu ya kero mbalimbali za Serikali kushindwa kupambana na watumishi wasio wema na wabadhirifu, mafisadi, wala rushwa na wahujumu uchumi‘ ‘Vita hii tumekuwa tukipigana sisi wanyonge na baadaye ikaungwa mkono na makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa, Sasa tumempata Rais Magufuli anayefanya kazi bila kuchoka kuifikisha Tanzania tunakokutaka, wanasiasa hao wamegeuka na wanaanza kumhujumu‘ ‘Tumeshangazwa zaidi tunaposoma na kusikia katika vyombo vya habari baadhi ya wanasiasa wakianza kumkejeli Rais Magufuli eti anaendesha nchi kinyume cha sheria na kuipeleka katika utawala wa kiimla‘ ‘Ni kwasababu hii, sisi wazalendo tunasema hoja za wanasiasa na wasomi kusema Rais...