TWANGA PEPETA KUZINDUA ALBAMU YA 13 MWANZA JUMAMOSI, KUCHANGIA MADAWATI
Mkurugenzi wa bendi ya African Stars, Asha Baraka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na uzindua albamu yake ya 13 ijulikanayo kwa jina la Husiyaogope Maisha mkoani Mwanza kwenye ukumbi wa Villa Park Jumamosi Mei 28. Kulia ni mwimbaji wa bendi hiyo, Haji Ramadhani. Bendi ya muziki ya African Stars “Twanga Pepeta” itazindua albamu yake ya 13 ijulikanayo kwa jina la Usiyaogope Maisha mkoani Mwanza kwenye ukumbi wa Villa Park Jumamosi. Akuzungumza jijini jana, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi huo yamekwisha kamilika na wanamuziki wake wapo kwenye maandalizi ya mwisho kwa ajili ya uzinduzi huo. Mbali ya wimbo wa Husiyaogope Maisha uliotungwa na Ali Choki, nyimbo nyingine zinazounda albamu hiyo ni Ndoa (Luizer Mbutu), Uso Chini, (Choki), Michepuko (Msafiri Diouf), Mapenzi Yanaumiza (Haji Ramadhani) na Ganda la Mua uliotungwa na Saleh Kupaza ambaye kwa sasa hayupo kwenye bendi hiyo. Asha ...