Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya adabu zake

Makala kuhusu Funga ya Ramadhan, hukumu, fadhila, adabu zake

Picha
Utangulizi Sifa zote njema zinamstahikia Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na sala na salamu zimfikie Mtume wake (Swalla Allahu alayhi Wasallam) pamoja na ndugu na maswahaba zake. Baada ya kumshukuru  Allah (Subhaanahu Wata’ala)  na kumtakia rehma na amani Mtume Muhammad (Swalla Allahu alayhi Wasallam) pamoja na ndugu zake na maswahaba zake wote, basi kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu (Subhaanahu Wata’ala)  amejaalia kwa waja wake  miongo [misimu] ya kuzidisha ndani yake matendo mema  na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala)  huzidisha pia malipo ya matendo hayo kwa waja wake, na miongoni mwa miongo hiyo ni huu  mwezi mtukufu wa Ramadhani. Basi katika makala haya nitaelezea kwa ufupi juu ya funga na yale yanayoambatana nayo ikiwa ni pamoja na  hukumu, fadhila na adabu zake. Ninamwomba Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)  awanufaishe Waislamu kwa yale nitakayoyaelezea, na aturuzuku ikh-laswi [kutaka radhi zake pekee] katika matendo yetu yote,  ...