Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya ALICHOSEMA KOCHA MSOLLA BAADA YA PENATI YA ALLY MUSTAPHA ‘BARTHEZ

ALICHOSEMA KOCHA MSOLLA BAADA YA PENATI YA ALLY MUSTAPHA ‘BARTHEZ

Picha
Na Baraka Mbolembole Kocha mkuu wa zamani wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) Prof. Mshindo Msolla alikuwepo katika uwanja wa Majimaji, Songea wakati mabingwa wa ligi kuu Bara, Yanga SC waliposawazisha kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya mwisho ya mchezo na kupata sare ya kufungana magoli 2-2 dhidi ya wenyeji, Maji Maji FC katika mchezo wa kufunga msimu wa 2015/16. Msolla pamoja na kuzungumzia uamuzi wa mwamuzi kutoa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Majimaji kuunawa mpira katika eneo la hatari pia anazungumzia mambo mengine manne ambayo ameyaona kwa msimu mzima. MAKOSA YA MWAMUZI “Maji Maji 2-2 Yanga: Kwa kweli sikuona makosa ya mwamuzi, mechi haikuwa na presha, nadhani ni malalamiko tu ya mashabiki ambao wanataka lazima timu ya nyumbani ishinde. Lakini waangalie ‘fair play,’ utashinda sawa kwa sababu unachezea nyumbani? Sikuona makosa ya mwamuzi katika mechi hii.” KIWANGO CHA UCHEZAJI “Kiwango ni kizuri na niseme kwamba vipaji bado vipo. Beki n...