SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 23 Mei 2016

T media news

ALICHOSEMA KOCHA MSOLLA BAADA YA PENATI YA ALLY MUSTAPHA ‘BARTHEZ

Na Baraka Mbolembole

Kocha mkuu wa zamani wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) Prof. Mshindo Msolla alikuwepo katika uwanja wa Majimaji, Songea wakati mabingwa wa ligi kuu Bara, Yanga SC waliposawazisha kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya mwisho ya mchezo na kupata sare ya kufungana magoli 2-2 dhidi ya wenyeji, Maji Maji FC katika mchezo wa kufunga msimu wa 2015/16.

Msolla pamoja na kuzungumzia uamuzi wa mwamuzi kutoa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Majimaji kuunawa mpira katika eneo la hatari pia anazungumzia mambo mengine manne ambayo ameyaona kwa msimu mzima.

MAKOSA YA MWAMUZI

“Maji Maji 2-2 Yanga: Kwa kweli sikuona makosa ya mwamuzi, mechi haikuwa na presha, nadhani ni malalamiko tu ya mashabiki ambao wanataka lazima timu ya nyumbani ishinde. Lakini waangalie ‘fair play,’ utashinda sawa kwa sababu unachezea nyumbani? Sikuona makosa ya mwamuzi katika mechi hii.”

KIWANGO CHA UCHEZAJI

“Kiwango ni kizuri na niseme kwamba vipaji bado vipo. Beki namba 3 wa Maji Maji-Sam Luhava ni mchezaji mzuri ambaye anapasaswa kutazamwa hadi katika timu ya Taifa.”

VIWANJA

“Kwa kweli viwanja vinapaswa kuboreshwa,vifanyiwe kazi ili viwe na ubora. Vinaharibu sana ladha ya mpira”.

USHINDANI

“Ukiangalia idadi ya pointi za Simba, Azam na Yanga na ukiangalia pointi za timu 6 za mwisho, gepu ni kubwa. Maana yake ni kwamba timu hazijiandai vizvri. Kwa hiyo ushauri wangu ni kwamba timu lazima zijiandae. Huwezi kushindana katika ligi kama haujajiandaa. Ushauri wangu kwa timu ambazo zimeokoka kushuka safari hii, zihakikishe zinajipanga vizuri vingenevyo ushindani hakuna.”

TIMU 5 TU ZILISHINDANA

“Ushindani wa ligi kiujumla hakuwa mzuri sana. Ulionekana mzuri kwa baadhi ya timu tano za juu (Yanga, Azam, Simba, Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar,) timu nyingine walikuwa washiriki.

NB; Kwa ukaribu zaidi, tafadhali unaweza ku-LIKE PAGE yangu BSports. Utapata Updates za michuano mbalimbali. Asanteni.