SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 23 Mei 2016

T media news

JEREMIAH JUMA & ELIUS MAGULI WAFUNGAJI BORA WAZAWA VPL, MGOSI & BARTHEZ…

Na Baraka Mbolembole

Amis Tambwe ameshinda tuzo binafsi ya mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara 2015/16. Raia huyo wa Burundi amefunga jumla ya magoli 21. Mganda, Hamis Kiiza anafuatia katika chati hiyo baada ya kufunga magoli 19 na orodha ya wafumania nyavu watatu bora inafungwa na Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye katika msimu wake wa kwanza VPL amefanikiwa kufunga magoli 17.

Tatu Bora ya wafungaji haina mchezaji  raia wa Tanzania na badala yake majina yao yanaanzia katika nafasi ya nne ambako nyota wawili wa Taifa Stars, Elius Maguli wa Stand United ya Shinyanga na Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons ya Mbeya wamefunga-kila mmoja amefunga magoli 14.

Si haba hasa ukizingatia washambuliaji hao hawachezi katika timu za Yanga, Azam ama Simba ambako wanacheza Tambwe, Ngoma (Yanga) Kiiza (Simba.) Katika orodha ya wafungaji bora kumi wa kwanza, raia wa kigeni wamechomoza wanne tu hii inamaanisha kwamba hata wachezaji wazawa walifanya kazi nzuri katika ufungaji na wanastahili kusifiwa.

Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast ameifungia timu yake ya Azam magoli 11 ndiye anayewafuatia Maguli na Jeremiah.

Atupele Green wa Ndanda SC amemudu kufunga magoli kumi. Mfungaji bora wa msimu uliopita, Saimon Msuva amemaliza msimu kwa kufunga magoli 9. Nahodha wa Azam, John Bocco, mshambuliaji kinda wa Simba, Ibrahim Ajib pia wamemaliza msimu kwa kufunga magoli 9 kila mmoja.

Mlinzi pekee kuingia katika orodha ya wafungaji kumi bora wa kwanza ni, Shomari Kapombe wa Azam FC ambaye amefunga magoli 8.

Wakati nahodha wa Simba, mshambulizi, Musa Hassan Mgosi akifunga goli lake pekee msimu wa 2015/16 katika game ya mwisho waliyopoteza 2-1 dhidi ya JKT Ruvu, kipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’ naye akafunga kwa mkwaju wa penalti na kuisawazishia timu yake dakika za mwisho katika sare ya 2-2 dhidi ya Maji Maji FC.

NB; Kwa ukaribu zaidi, tafadhali unaweza ku-LIKE PAGE yangu BSports. Utapata Updates za michuano mbalimbali. Asanteni.