Rais Magufuli: Huyu Shetani Aliyetulaani Watanzania kwanini Asife? Hivi Hatuhurumii hata Kidogo?
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) limetakiwa kuingia ubia na kampuni za madini nchini ili kutengeneza ajira kwa vijana wa Kitanzania ambao wengi wao wako vijiweni. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Rais John Magufuli wakati akizindua majengo ya mifuko ya pensheni ya NSSF na PPF yaliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 60 yaliyojengwa jijini hapa. Rais Magufuli alisema wakati umefika kwa NSSF kujikita katika biashara ya kupata faida kwa haraka kama vile ya madini ya tanzanite kwa kuanzisha viwanda vya kukata madini hayo na kusanifu ili vijana wafundishwe na hatimaye kuajiriwa katika viwanda hivyo. Alisema suala la Tanzania kuwa nchi ya tatu duniani kwa kuuza madini ya tanzanite wakati madini hayo yanapatikana hapa hapa tu na kuziacha nchi za India na Kenya zikiongoza, ni suala la kushangaza sana. Alisema NSSF sasa inapaswa kujipanga na kuingia katika biashara ya madini hususan tanzanite kwa kuingia ubia na kampuni kama hiyo ya Signature inayomilikiwa na mzawa Sailesh Pandit ili ifan...