Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya BAADA YA UCHAGUZI KUMALIZIKA

BAADA YA UCHAGUZI KUMALIZIKA, HUU NDIYO MSIMAMO WA TFF KUHUSU RAIS MPYA WA FIFA

Picha
Shirikisho la soka barani Afrika CAF lilitoa tamko kabla ya uchaguzi wa rais wa FIFA kwamba, Afrika pamoja na vyama vyake vya soka vitamuunga mkono Sheikh Salman katika kinyang’anyiro hicho kilichofanyika February 26, 2016. Mbali na CAF kutoa agizo kwa vyama vyake vya soka kumuunga mkono Sheikh Salman bado mgombea huyo alishindwa kufurukuta mbele ya Gianni Infantino ambaye alishinda kiti hicho cha urais kwa tofauti kubwa ya kura na kuashiria huenda kuna nchi wanachama wa CAF hawakumchagua Sheikh Salmani. Shaffihdauda.co.tz imefanya mahojiano maalumu na rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi kutaka kujua hasa ni kitu gani kimemuangusha Sheikh Salman licha ya Afrika bara lenye kura nyingi kutangaza kumuunga mkono rais huyo wa shirikisho la soka la Asia. “Tumepata rais mpya wa FIFA sasa Gianni Infantino nimeongea na waandishi wa habari wa kimataifa na sasa naongea na Clouds TV, Clouds FM na shaffihdauda.co.tz ni kwamba tumekubali matokeo ya uchaguzi, uchaguzi ni uchaguzi kikubwa sas...