Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mchango wa Ndg. Zitto Kabwe Bungeni 28 Aprili 2016.......Kazirudisha Upya hizi Tuhuma mbili za Rushwa

Mchango wa Ndg. Zitto Kabwe Bungeni 28 Aprili 2016.......Kazirudisha Upya hizi Tuhuma mbili za Rushwa

Picha
Mheshimiwa Spika, Tangu tuanze Mkutano huu wa Bajeti mwaka 2016 kumekuwa na malalamiko kutoka kwa Wabunge na hasa wabunge wa kambi ya Upinzani Bungeni kuhusu ukiukwaji wa Sheria mbalimbali za nchi katika masuala ya Bajeti.  Jana jioni Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Andrew Chenge alitoa Changamoto kuwa Wabunge tuseme ni sharia gani zimekiukwa katika mchakato mzima wa Bajeti ya Nchi hivi sasa. Kwa maoni yangu, kuna ukiukwaji kadhaa wa sharia ya Bajeti, sharia namba 11 ya mwaka 2015 katika mchakato wa Bajeti ya Mwaka huu. Nitaeleza kwa ufupi. Mheshimiwa Spika, kifungu cha 8 cha sheria ya Bajeti kinaeleza namna ambavyo mfumo wa Bajeti ya Serikali unapaswa kuwa.  Vifungu cha 8(1)(b) na 9(1)(a) na 19(1) vinaeleza namna mchakato wa Bajeti unavyopaswa kuwa. Vifungu hivi vinataka “Planning and Budget Guidelines” zipitishwe na Bunge katika mkutano wake wa Mwezi Februari kila mwaka. Sheria inataka “budget ceilings” ziidhinishwe na Kamati ya Bajeti na baadaye ...