Vituko Kumi Ambavyo Havitasahaulika vya Marehemu Lucy Kibaki...
IJUMAA iliyopita uvumi ulienea kuhusu mahali alikokuwa Mama Lucy Kibaki, aliyekuwa mke wa rais mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, ambapo vyombo vya habari vilieleza kwamba alikuwa amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali moja jijini Nairobi. Mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 75 alikuwa haonekani sana hadharani tangu mwaka 2010 na kutokuwepo kwake kulionekana wazi baada ya kutohudhuria hafla ambapo mumewe, Rais Kibaki, alikabidhi madaraka kwa Uhuru Kenyatta mwaka 2013. Yote kwa yote, taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya Rais Uhuru Kenyatta ilisema mama huyo alifariki jana katika hospitali moja jijini London, Uingereza, alikokuwa anapatiwa matibabu na kwamba mipango ya mazishi yake ilitegemewa kutangazwa baadaye. Lucy Yafuatayo ni matukio kumi ambayo yalimhusisha mama huyo ‘mcharuko’ aliyekuwa hawezi kujizuia anachotaka kukisema ama kukifanya: Miezi kadhaa baada ya mumewe kuapishwa kuwa rais wa ta...