Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Nafasi ya Mkurugenzi Mkuu NSSF ni Moto...Yakaa Siku 22 Bila Mkurugenzi wala Kaimu wake

Nafasi ya Mkurugenzi Mkuu NSSF ni Moto...Yakaa Siku 22 Bila Mkurugenzi wala Kaimu wake

Picha
Nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) inaonekana kuwa moto baada ya mfuko huo kumaliza siku ya 22 bila ya kuwa na mbadala wa Dk Ramadhan Dau au kaimu wake. Jaribio la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama kuziba nafasi hiyo kwa muda lilidumu kwa saa tano tu baada ya kulazimika kutengua uteuzi wa Carina Wangwe Alhamisi iliyopita. Waziri Mhagama alilazimika kutengua uteuzi huo kwa maelezo kuwa taratibu zilikosewa huku Balozi Ombeni Sefue akieleza kuwa mkurugenzi huyo wa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Jamii (SSRA) alitakiwa kuwa msimamizi tu na si kaimu mkurugenzi. Jana, juhudi za gazeti hili kutaka kujua maendeleo ya uteuzi wa mtu mpya wa kushika nafasi hiyo ziligonga mwamba. Balozi Sefue, ambaye hadi jana alasiri alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi, hakutaka kuzungumzia suala hilo akimuelekeza mwandishi kumtafuta Waziri Mhagama. Lakini Waziri Mhagama hakuweza kupatikana licha ya kutafutwa mara kadhaa. Juhudi za kumpata kwa simu zili...