Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Serikali Kununua Magari Mengi Zaidi ya Polisi

Serikali Kununua Magari Mengi Zaidi ya Polisi

Picha
Serikali imepanga mwaka ujao wa fedha kununua magari  mengi kwa ajili ya kuyasambaza kwenye vituo tofauti vya Polisi nchini vyenye uhaba. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema mpango huo utatekelezwa katika bajeti ya mwaka 2016/17. Alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Igalula, Musa Ntimizi (CCM), aliyehoji kama wizara haioni umuhimu wa kuvipatia magari vituo vya polisi ambavyo havina magari katika jimbo hilo ili kurahisisha utendaji kazi. Mbunge huyo pia alitaka wizara kumalizia ujenzi wa kituo cha polisi kikubwa kilichojengwa katika kata ya Loya halmashauri ya Tabora (Uyui) ambapo kwa sasa wananchi wameishiwa nguvu ya kuendeleza ujenzi huo. Waziri alisema, serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na wananchi katika kuchangia maendeleo, alimtaka mbunge huyo kuwasiliana na wizara yake ili waweze kuona namna ya kusaidia kumalizia ujenzi wa kituo hicho ili kianze kufanya kazi. Katika swali la msingi, mbunge huyo alitaka kufahamu ni lini kituo cha...