Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya huku Asilimia 79 Zikiwa Salama

Asilimia 18 Ya Simu Za Kiganjani Zaonekana Ni Bandia ,huku Asilimia 79 Zikiwa Salama

Picha
MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa asilimia 79 ya simu za kiganjani zilizofanyiwa utafiti kwa kipindi cha desemba hadi February mwaka huu ziko salama na sio za bandia ,huku asilimia 18 zikionekana zikiwa za bandia hivyo kuwataka wananchi kutambua kuwa simu feki zilizoko sokoni ni chache tofauti na kipindi cha nyuma. Pia imebainika kuwa asilimia kubwa ya nyumba zinazoungua na umeme ni kutokana na simu bandia ambazo betri zake au vifaa vyake hushindwa kuhimili  mionzi pindi zinapokuwa zinachajiwa hivyo kusababisha mlipuko wa moto na hivyo kuleta madhara . Hayo yalisemwa na meneja uhusiano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania Innocent Mungi alipokuwa akizungumza katika semina ya mfumo wa rajisi ya  namba za utambulisho wa simu za kiganjani iliyowashirikisha wadau na wafanyabiashara wa jijini hapa. Alisema kuwa kutokana na elimu ambayo wameitoa kwa wafanyabiashara wa simu  hizo ya kuhakiki kwanza kabla ya kuwauzia wananchi imepunguza uingizaji wa simu feki...