Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Lady Jaydee Kufunga Ndoa Tena Baada ya Kupewa Talaka na Gadner

Lady Jaydee Kufunga Ndoa Tena Baada ya Kupewa Talaka na Gadner

Picha
Siku chache baada ya kupewa talaka na aliyekuwa mumewe, mtangazaji Gardner G. Habash ‘Captain’, mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva anayekuja na ujio mpya alioubatiza jina la Naamka Tena, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide amedaiwa kupata mwanaume mwingine ambaye yupo kwenye mikakati kabambe ya kumuoa, Risasi Jumamosi lina ubuyu kamili. Jide ambaye amekuwa kimya kimuziki kwa zaidi ya miaka miwili, Februari mwaka huu alipewa talaka katika Mahakama ya Manzese-Sinza jijini Dar baada ya mvutano uliodumu kwa muda mrefu tangu wawili hao washindwe kuishi pamoja. Kwa mujibu wa chanzo makini, Jide alimpata mwenza muda mrefu tangu walipomwagana na Gardner lakini mipango ya ndoa ikashindwa kwenda haraka kwa sababu hakuwa amepewa talaka hiyo aliyoidai mahakamani. “Mbona Jide kitambo tu alishapata mtu sema alikuwa hawezi kufanya mambo ya ndoa kwani hakuwa amepewa talaka na Gardner ila sasa hivi yupo huru na mwaka huuhuu huenda kikaeleweka,” kilisema chanzo hich...