Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Waziri Mkuu Aongoza Wakazi Wa Dodoma Mazishi Ya Askofu Isuja wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma

Waziri Mkuu Aongoza Wakazi Wa Dodoma Mazishi Ya Askofu Isuja wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma

Picha
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya waumini na wakazi wa mkoa wa Dodoma katika mazishi ya Mhashamu Askofu Mstaafu, Mathias Isuja wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma. Amesema kifo hicho ni pigo kwa watu wote na si kwa kanisa pekee kwa sababu walimtegemea kulisaidia Taifa kiroho na kimaendeleo. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 20, 2016) wakati akizungumza na waumini na wakazi wa mkoa huo na mikoa jirani kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiaskofu la Mtume Paulo wa Msalaba mjini Dodoma. Askofu Isuja ambaye alizaliwa Agosti 14, 1929 alikuwa Askofu wa kwanza mzalendo katika Jimbo la Kanisa Katoliki la Dodoma. Alistaafu kazi ya uaskofu mwaka 2004 kwa mujibu wa sheria ya kanisa. Alifariki Aprili 13, mwaka huu. Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kumuenzi Askofu Isuja kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa uhai wake na kuyaendeleza yote aliyoyaanzisha kwenye maeneo aliyowahi kuyatumikia. “Tumepoteza mtu makini, sisi ni mashahidi ...