AVEVA KATOKA HADHARANI KUANIKA SABABU 4 ZILIZOINYIMA SIMBA VPL
Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva (kulia) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu Simba kuboronga kwenye mashindandao ya msimu huu (VPL na FA Cup) kushoto ni Haji Manara-ofisa habari wa Simba Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva leo May 18 amejitokeza mbele ya waandishi wa habari na kutoa sababu kadhaa ambazo kwa namna moja au nyingine zimeifanya klabu yao kukosa ubingwa VPL kwa mara nyingine tena ikiwa ni msimu wao wan ne mfululizo bila kutwaa taji hilo. Katika hotuba yake kwa wanahabari, Aveva amekiri kwamba malengo yao waliyojiwekea ya kutwaa ubingwa FA Cup na VP yamekwama kwa kushindwa kuchua kombe hata moja kati ya hayo. Badala yake akatumia muda mwingi kueleza sababu ambazo zimefanya Simba kushindwa kufanya vizuri kwenye ligi. Wachezaji wameiangusha Simba “Kuna wanajeshi ambao hawakuwa tayari kulitumikia jeshi la Simba kwa mfano, kuna mchezaji ambaye kwa makusudi au kwasababu za kimchezo alifanya makosa akafungiwa kutokana na kanuni za mchezo na sisi ...