Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CUF Yataka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Aombe Radhi

CUF Yataka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Aombe Radhi

Picha
Chama cha Wananchi(CUF) kimemtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awaombe radhi watanzania kwa kuwadhalilisha kuwa hawapendi kufanya kazi, badala yake  wanashinda kuangalia Bunge, hali ambayo imeisababisha lisirushwe moja kwa moja. Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF Taifa, Twaha Taslima amesema Waziri Mkuu alitoa tuhuma hizo kwa wananchi akiwa nchini Marekani hivi karibuni,wakati  siyo kweli kwamba watanzania wanakesha kuangalia bunge tangu  linapoanza hadi linakwisha bila kufanya kazi. Hivi karibuni Waziri Majaliwa akizungumza na watanzania waishio Uingereza alisema sababu ya bunge kutorushwa moja kwa moja ni kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ “Kama ni hivyo basi maisha ya watanzania wengine yangekwama hivyo Serikali ya awamu ya tano kazi yake kubwa sasa ni kutaka kuwarudisha watanzania kwenye woga wa kutoiwajibisha Serikali kwa kisingizio cha hapa kazi tu slogani hii ni ya kuua demokrasia,”  amesema Taslima. Taslima ameyasema hayo ...