Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya WASANII BONGO WAAMUA KUREJESHA ENZI ZA TAMTHILIA

WASANII BONGO WAAMUA KUREJESHA ENZI ZA TAMTHILIA, HIZI NI TATU KUTOKA KWA RAY, J B NA JOHARI NA IRENE UWOYA

Picha
Tamthilia za kwenye runinga zimetengeneza mzizi wa filamu za Tanzania. Kwa lugha nyingine, kama kusingekuwepo na maigizo ya kwenye TV, pengine kusingezaliwa mastaa wengi wa filamu tulionao sasa. Karibu asilimia 80 ya waigizaji wa filamu wanaofanya vizuri hapa kwetu wametokea kwenye vikundi vya maigizo vilivyokuwa vikirusha vipindi vya kwenye TV, hususan, ITV enzi hizo. Mastaa kama marehemu Steven Kanumba, Ray Kigosi, JB, Johari, Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Single ‘Rich’ Mtambalike’, Monalisa, Mzee Chilo, Bi. Hindu, Cloud, Dr Cheni na wengine, walianza kujipatia umaarufu kwenye tamthilia. Vikundi kama Kaole Sanaa Group, Kidedea, Mambo Hayo na vingine vilichangia kwa kiasi kikubwa kukomaza vipaji vya uigizaji walivyokuwa navyo wasanii wengi.  Enzi hizo malipo waliyokuwa wanapata wasanii kupitia tamthilia zao yalikuwa duni na hayakuweza kuwafaidisha kwa lolote. Wengi walifanya kwa passion na wale waliostahimili walikuja kuanza kula matunda baada ya ...