Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Malori ya Kubeba Mizigo Kuondolewa Dar....Trilioni 1 Yatengwa Kwa Kazi Hiyo

Malori ya Kubeba Mizigo Kuondolewa Dar....Trilioni 1 Yatengwa Kwa Kazi Hiyo

Picha
Malori  ya kubeba mizigo, ambayo yamekuwa yakichangia msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa jijini Dar es Salaam, yanatarajiwa kuondolewa mara tu reli ya kisasa ‘Standard Gauge’, iliyotengewa Sh trilioni moja katika Bajeti ya Serikali, itakapofika Ruvu mkoani Pwani.  Rais John Magufuli amesema hayo jana wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kwanza ya juu (Flyover) nchini Tanzania, inayojengwa katika makutano ya Barabara ya Mandela na Barabara ya Nyerere eneo la Tazara, kwa ufadhili wa Serikali ya Japan.  Barabara hiyo ya juu kwa mujibu wa taarifa za Wakala wa Barabara (Tanroads), ikikamilika inatarajiwa kupunguza muda wa magari kukatiza katika makutano hayo kwa asilimia 80, kutoka wastani wa dakika 45 hadi dakika 10 tu kwa wanaotoka upande mmoja kwenda mwingine.  Akifafanua zaidi kuhusu reli, Rais Magufuli alisema fedha hizo zimetengwa katika bajeti itakayopelekwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanz...