Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Nchi tano zinazoongoza kwa ufisadi duniani

Nchi tano zinazoongoza kwa ufisadi duniani

Picha
Nchi tatu za Afrika zimetajwa kwenye orodha ya nchi tano zilizokithiri kwa vitendo vya rushwa duniani katika ripoti ya Shirika la kimataifa Transparence iliyotolewa hivi karibuni. Takwimu za Transparent International zilizotolewa mapema mwaka huu, zimeiweka Tanzania katika nafasi ya 117 duniani. Miongoni mwa nchi tano zinazoongoza, mataifa ya Bara la Afrika, Somalia, Sudan na Sudan Kusini yametajwa. Somalia lililo katika pembe ya Afrika, ambayo imekuwa bila Serikali ya kitaifa tangu mwaka wa 1991, ndiyo taifa linaloongoza kwa ufisadi kwa kushika nafasi ya 167 ikifungana na Korea Kaskazini, Sudan Kusini likishika nafasi ya 163 kwa kufungana na Angola, Sudan ikiwa nafasi ya 165. Nchi nyingine iliyo katika nafasi tano za juu kwa rushwa na ufisadi duniani ni Afghanistan iliyo na alama 166. Katika ukanda ya Afrika Mashariki, Burundi inaongoza kwa kiwango cha juu rushwa na ufisadi ikiorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani kwa kupata jumla ya alama 21. Uganda na Kenya zimetoshana katik...